'Mama bila leso!' Willy Paul amwita Ringtone baada ya kuzidi kumzungumzia

Saa chache baada ya msanii Willy Paul na Ringtone kurushiana matusi na cheche za maneno katika mtandao wa kijamii, Willy Paul hakutosheka na yale aliomtusi msanii huyo huku akizidi na matusi yake.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram, Willy aliposti ujumbe akimshauri Ringtone aende akashindane na wamama kama msanii Akothee.

Huu hapa ujumbe wa kwanza ambao uliwafanya wawili hao kurushiana maneno. Ijapokuwa wameokoka je wanapaswa kuwapa mashabiki mfano mwema au tabia za vijana wa mtaani wasio na mwelekeo?

“MATAKO WEWE RINGTONE @ringtoneapoko THE FACT THAT NIMETULIA ISIFANYE UONE KAMA MIMI NI UR FELLOW WOMAN!!! BLOODY NA UACHANE NA NADIA MUKAMI.. TOA WIMBO YAKO TUONE SHENZI, #NIKUNE IS A HIT AND UR LIFE IS A MISSSSS!!” alisema Willy Paul.

Willy paul hakutosheka na cheche za maneno yake na kupitia mtandao wake wa kijamii alimuonya ringtone na kumwambia yeye ni mama bila leso.

Ujumbe huo ni kama vile ufuatavyo;

", mama bila leso...So this stupid man is still talking about me? Naona nikitandika huyu mkisii!! You are a disgrace to the Kisssiiii people!! Remember kelele yako haitazuia Kuenda.:: check the views and trend on YouTube alafu umeze wembe!!" Willy Aliandika.

Je wawili hao wana maadili mema kwa mashabiki wao hata baada ya kupewa pesa na rais Uhuru Kenyatta kwa sababu ya janga la corona?