Mama kahaba awaacha watoto Kakamega na kutoweka

Wakazi wa mtaa wa little home viungani mwa mji wa Kakamega wanawataka polisi kuchunguza na kumkamata mama mmoja anayefanya biashara ya ukahaba ambaye amewaacha watoto wake wanne kwa chumba na kutoweka kwa miezi miwili sasa.

Mmiliki wa nyumba hiyo Marygoet Miheso ameshangazwa na kitendo cha mama huyo aliyewaacha watoto wa miaka kumi na mitatu, kumi na miwili, miaka saba na miezi sita bila chakula.

Hayo yakijiri, wakazi wa eneo la Murumba lililoko butsotso mashariki lurambi katika kaunti ya Kakamega wameitaka serikali kuingilia kati na kukomesha wizi wa mifugo unaoendelezwa na kundi moja la wezi

Wamesema ng’ombe wao wanaibiwa na kuchinjiwa ktika kituo kimoja kabla ya nyama kuuzwa mjini kakamega.