Baby mama wa Bahati na dadake walinishambulia adai Diana Marua

Diana Marua mkewe msanii wa nyimbo za kumtukuza Mungu Bahati alifichua kwa mara ya kwanza jinsi mama Mueni, Yvette Obura na dadake walimshambulia kupitia mtandao wa kijamii.

Hii ni baada ya kuweka picha ya Mueni katika mtandao wa kijamii mtoto ambaye Bahati alizaa na Yvette Obura.

Diana aliendelea kusema kwamba yeye ni mama ya watoto watatu Morgan, Heaven na Bahati kwa sababu ya mashambulizi hayo na bado anampenda mtoto Mueni sana.

"Mliniuliza nimweke katika mtandao wa kijamii, na nikafanya jinsi mlivyokuwa mnataka, nilimueka kwa roho safi kwa sababu Mueni hana hatia yoyote, Lakini mnajua kilichofuatia baada ya kumweka." Alieleza Diana.

Aliongeza,

"Baada ya picha hiyo nilishambuliwa vibaya sana na mamake Mueni Yvette Obura na dada yake katika mtandao wa kijamii na kejeli zingine nyingi. Mueni si mtoto wangu katika mitandao ya kijamii." Alisema Diana.

Alifichuwa kuwa ni yeye alimfungulia Mueni akaunti ambayo amemzuia mamake mzazi kumfuata katika mitandao ya kijamii.

Bahati akiongea katika onyesho la 'Bahati reality' alisema alimzuia Yvette kumfuata mwanawe katika mitandao ya kijamii kwa sababu hakumpa heshima na hata kumshukuru.

"Hujui mbona nili kublock? sasa kama mtu hajui kwanini nilimblock si hakuna haja ya hii meeting. Kama Vyette naamka leo tuko sawa.

Kidogo watu wametuona kwa Bahati Reality usiku, asubuhi najipata niko katika mitandao kama vile blogu, kuna saa Vyette ameniweka katika mablogu for no  good reasons.

Hadi nikaanza kudhani anafanya kazi huko, sasa utafanya aje ili usione huyu mtu,si unamblock, mimi naongeanga na shosho yake.

I'll do anything to make sure my daughter gets the best life that have never had, siku ya fathers day for example ameamka ameambia mtoto oh hi my daughter happy fathers day to me.

Because I'm your father sasa mimi nmekaa kwa hii meeting kama uncle ama relative? Alieleza Bahati.