diamondsmumandherbenten

Mamake Diamond Platnumz ampasha Jones kisa mpango wa kando

Mamake staa wa Tanzania Diamond Platnumz , Sandra amepandwa na hasira baada ya kugundua Rally Jones ambaye ni mpenzi wake anatoka kimapenzi na mwanamke mwingine.

 Inadaiwa kuwa Rally Jones amemuweka mimba mwanadada kwa jina Sharifa bila ufahamu wa mamake Diamond.
Katika kipande cha sauti  kinachosambaa katika mitandao ya kijamii, Sandra anasikika akimkashifu na kumkaripia mpenzi wake Jones katika mazungumzo ya simu na mwanahabari kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Sina Mpango wa Kando! Tanasha Donna awaambia mashabiki

Katika kipande cha kile cha sauti, mama huyu mwenye utata anasikika akisema kuwa bado anampenda Rally Jones na wameoana kirasmi.

Sandra anaongeza kusema kuwa hapigwi moyo kabisa na kitendo kiovu cha mpenzi wake kuzaa nje ya mahusiano na mwanamke mwingine na kumwambia kuwa kama anahitaji watoto zaidi aendelee  kufanya hivyo.

 

Tumekusongezea mazungumzo hapa:

Mwanahababari: Ulisikia habari za mwanamke aliyezaa naye?

diamondwearingyellow

Sandra: Simjui aliyezaa hata kama kazaa sio mke, mimi ni mke najulikana kote. Kama anataka azae tu, hakatazwi mtu kuzaa halafu mimi sio tasa, watoto ninao na tena wanajulikana dunia nzima. Wanalinufaisha jiji, sasa mimi mtoto wake atanishughulisha nini? Ndio kwanza mchanga kama kazaliwa. Hanibabaishi chochote hata kama ni mwanamke ako naye hanibabaishi. Hana mbele wala nyuma mimi sio muuza uchi. Mimi nakaa kwangu na nina familia na ninajiheshimu na nina kila kitu. Kama alichepuka akaenda kuzaa azae tu.

 

Toboa siri: Bibi anadhani nilifariki ila nimekuwa kwa mpango wa kando

Mwanahabari: Na mahaba yenu moto moto?

Sandra: Kama yote.

Mwanahabari: Safi sana safi sana…

Sandra: Ndio mimi mke hali wa ndoa akitokea mwingine feki.

Mwanahabari: Kumbe mlishafunga ndoa mama?

Sandra: Kama unapajua kwangu uje nikuonyeshe cheti cha ndoa.

Mwanahabari: Asante mama nakupenda.

Sandra: Umemaliza au unalingine unataka nikupe?

Mwanahabari: Nimemaliza mama, asante. diamondandhismom

Sandra: Haya wajue wanangu masupasta wanalitikisa jiji.

Haya yanatokea baada ya ubuyu mtaani kudokeza kuwa mama huyu wa miaka 52 ana ujauzito. Jones bado hajaweza kuzungumzia swala hili la kuzaa nje ya ndoa.
Hadithi imetafsiriwa na kuhaririwa na Abraham Kivuva

Photo Credits: courtesy instagram

Read More:

Comments

comments