Mambo usiyoyajua kuhusu maisha ya binadamu wa kawaida

Mwili wa binadamu una viungo vingi na mambo mengi sana na ambayo hata binaadamu mwenyewe hayajui. Kuna mambo kumi muhimu ambayo wengi hawayafahamu.

Ndani ya mwili wa binadamu mmoja, mna vijiumbe vingi kuliko hata watu walioko duniani wote.

Binadamu wa kawaida hawezi lamba kisugudi chake. Ulimi wa binadamu huwezi fikia kisuguzi chake hata uwe mrefu namna gani

Mtoto anapozaliwa huwa hana goti lake kamili. Yai la goti huwa halijamea kwani yai hili huanzia kumea kamili mtoto akiwa na umri wa miaka miwili.

Ulimi wa kila mtu ni tofauti na watu wengi,kama ilivyo kwa vidole vyote, ndimi pia huwa tofauti sana kwani kila mtu huwa na alama tofauti za ulimi.

Moyo wa binadamu wa kawaida hudunda mara zaidi ya elfu mia mioja kwa siku moja.

Wanaume wana uwezo wa hali ya juu kusoma maandishi ikilinganishwa na wanawake. Jambo hili ni kuwa wanaume hufunga macho mara moja wakati wanawake wakifunga mara mbili kwa sekunde moja

Baada ya kula chakula, mwili wa binadamu huchukua muda wa takriban masaa kumi na mawili ili kumaliza kusyaga chakula hicho.

Binadamu wa kawaida hulala baada ya dakika saba. Hata hivyo, wanawake wana uwezo wa kuskia mambo haraka kuliko wanaume.