Kulingana na Emily, ugonjwa wa Saratani uko katika nafasi ya tatu kwa magonjwa yanayoongoza kwa mauaji ya watu wengi kila siku. Ugonjwa wa saratani unasababisha vifo vya watu zaidi ya 90 kila siku hapa nchini Kenya.
Ochieng anasema kuwa kuna aina mbili kuu za Saratani 'Screenable na Unscreenable'. Saratani zinazogundulika kwa haraka ndizo Screenable na mfano mzuri ni saratani ya Matiti na Saratani ya Koloni.
Kulingana naye Emily, Ugonjwa wa saratani husababishwa na ukosefu wa kufanya mazoezi mwilini, ukosefu wa vyakula vyote (balanced Diet). Ulaji wa nyama kwa wingi pia huleta ugonjwa wa saratani kwani nyama nyekundu huongeza mafuta mwilini.
"Kila sehemu ya mwili inaweza kupata saratani na hivyo ningewaomba wakenya wafanyiwe uchunguzi kwani Saratani ikigundulika mapema inaweza kutibiwa," Emily anazidi kueleza.