Man Njoro amuomba Onyango kumlipia mpangaji wake kodi (VIDEO)

masaibu ya onyango
masaibu ya onyango
Katika kitengo cha masaibu ya Onyango ambacho huja kwako kila siku kabla ya patanisho, wanajambo hupata fursa ya kutizama au kuelewa uhusiano wa bwana Onyango na rafiki zake man Njoro na Wafula.

Wawili hawa huwa na tabia zisizoeleweka kwani leo mmoja wao ni mkarimu na kesho wanapigana au hata utawapata wanasaidiana kwa mambo fulani.

Hata hivyo, katika kitengo kimoja, bwana man Njoro ambaye ni mwenye nyumba alikuwa na mpango maalum wa kumweka Onyango mtegoni ili aweze kuilipia familia moja kodi ya nyumba bila kufichua kuwa yeye ndiye atakayepokea zile fedha.

Gidi alisimulia,

Man Njoro ambaye ni rafiki wa karibu wa Onyango amebisha mlangoni mwa Onyango huku akilia sana. Man Njoro anamwambia Onyango kuwa kuna familia moja wanateseka sana.

Aliongeza kuwa huyo mzee alipoteza kazi na sasa imetimia mwaka mmoja na hajafanikiwa kupata kazi, isitoshe mkewe pia hana kazi na hufanya vibarua hapa na pale na wawili hao wana watoto watano.

Sahii familia hiyo hawana chakula kwani hata mwenye nyumba naye yuko karibu kuwafurusha, na kwa sababu bwana Onyango ni mtu mwenye huruma kuu, alimwomba hata kama atawasaidia kwa kuwalipia kodi ya nyumba.

Onyango akafikiria na baada ya mda mchache akauliza kodi ni pesa ngapi na man Njoro akamweleza kuwa kodi ni pesa kidogo sana, shilingi elfu kumi na tano. Isitoshe kodi hiyo inatakikana siku inayofuata.

Hata hivyo, Onyango aliamua kuuliza maswali kadha wa kadha kabla ya kuisaidia familia ile, na kumuuliza Man Njoro kuhusu uhusiano wake na ile familia. Hapo ndipo Onyango alipigwa na butwaa pindi tu Man Njoro alipofichua kuwa yeye ndiye mwenye nyumba.

Tazama uhondo kamili,