Ed3gkWkWAAQN6Vh

Man United yaicharaza Leicester City na kufaulu miongoni wa timu 4 bora

Mechi kati ya Leicester City na Man United  iliochezwa mnamo tarehe 26 Julai iliwashuhudia Mashetani Wekundu kuingia kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya. Mabao mawili katika kipindi cha pili kutoka kwa Lingard na Fernandes yalitosha kuzima Leicester.

Leo ni siku ya kiama katika ligi kuu ya Uingireza

Man United wameshikilia nafasi ya tatu na pointi 66 huku wakifuatwa na timu ya Chelsea. Mechi hiyo ya mwisho ya msimu wa 2019/20 ilikuwa na kibarua huku pande zote zikipigania kumaliza kwenye nafasi ya nne bora.

Ed3sN8dWAAEd1Q_

Mashetani Wekundu walikuwa na imani kuwa droo itawatosha kuingia katika mashindano ya bara Ulaya licha ya matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Wolves. United walionekana kujivuta awamu ya kwanza katika uwanja wa King Power huku wenyeji wakitawala mechi hiyo.

FA Cup: Wanabunduki walipua Manchester City na kujikatia tikiti ya fainali

Awamu ya pili iliwashuhudia Foxes wakikaribia kutingisha wavu katika dakika ya 60 kupitia kwa Jamie Vardy ambapo juhudi zake zilikwishia kwenye mlingoti.

116167548_1452122724975672_2665813047775049143_o(1)

Matokeo hayo yana maana kuwa wenyeji hao wa Old Trafford watajiunga pamoja na Chelsea, Man City na Liverpool katika kinyang’anyiro cha Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kumaliza wa tatu kwenye jedwali.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments