Manchester City yapigwa marufuku ya kutoshiriki michuano ya UEFA

Manchester City wamepigwa marufuku ya kutoshiriki katika michuano ya bara Uropa, kwa misimu miwili ijayo. Hii ni kufuatia kupatikana na makosa yaukiukaji wa sheria ya matumizi ya fedha yaani Financial fair play.

Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza pia wamepigwa faini ya euro milioni 30.

Man City wapigwa marufuku ya kutoshiriki michuano ya UEFA

Hii inamaanisha kuwa Manchester City hawatoshiriki ligi ya mabingwa kwa msimu; 2020-2021 na 2021-22.

Kwa upande wao, Manchester City wametangaza kutoridhishwa ila kukiri kutoshtushwa na uamuzi huo. City wamesema kuwa watakata rufaa kuhusiana na uamuzi huo katika mahakama ya kuangazia maswala ya michezo.

|"Manchester City is disappointed but not surprised by today's announcement by UEFA Adjudicatory Chamber." Ujumbe kutoka klabu hiyo ulisema.

Waliongeza,

The club has always anticipated the ultimate need to seek out an independent body and process to impartially consider the comprehensive body of irrefutable evidence in suport of its position."