Manchester United wajiandaa kumnyakua Christian Eriksen Januari

Manchester United wanajiandaa kumnyakua Christian Eriksen kutoka Spurs mwezi Januari. Ole Gunnar Solskjaer hajakata tamaa baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa miaka 27 katika dirisha la uhamisho la msimu wa joto.

Eriksen alidai kutaka changamoto mpya mwishoni mwa msimu uliopita na alitaka kuhamia Real Madrid. Lakini uhamisho huo haukuwezakana kabla ya dirisha la uhamisho la Uhispania kufungwa jana na kuwacha nafasi ya United kumsajili mwezi Januari.

Kiungo wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka amejiondoa kutoka kwa kikosi cha Uingereza kutokana na jeraha la mgongo. Wan-Bissaka alitajwa kwa kikosi cha Gareth Southgate kwa mara ya kwanza kwa mechi yao ya kufuzu kwa michuano ya Euro mwaka 2020 dhidi ya Bulgaria na Kosovo.

Taarifa kutoka Uingereza zinasema mchezaji huyo wa miaka 21 ameregea kwa timu yake kutokana na jeraha la mgongo. Hakuna aliyepangiwa kuchukua nafasi yake kwani Trent Alexander-Arnold na Kieran Trippier tayari wapo kwenye kikosi hicho. Uingereza itachuana na Bulgaria jumamosi ugani Wembley kabla ya kupambana na Kosovo siku tatu baadae.

Alexis Sanchez anasema hajutii kujiunga na Manchester United lakini anasema hakuwa na muda mzuri wa kucheza kufana.

Raia huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Inter Milan kwa mkopo wa msimu mmoja mwezi Agosti baada ya miezi 19 Old Trafford. Alikua mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi United, takriban elfu 400 kwa wiki lakini alifunga mabao matano tu katika mechi 45 baada ya kujiunga kutoka Arsenal January mwaka wa 2018.