Wamedaiwa kukosa kulipa kodi ya shilingi milioni 38,692,694 katika taehe tofauti kati ya mwaka wa 2010 na 2015 wakiwa momabasa kama wakurugenzi wa Giche Ltd, zilizofaa kutozwa kutoka kwa mapato yao pamoja na faini .
Wakili wa serikali Annette Wangia hakupinga kuachiliwa kwao kwa dhamana lakini akaitaka mahakama kuangazia uzito wa mashtaka dhidi yao .
Hakimu mkuu Lawrence Mugambi aliwaachilia kwa dhamana ya shilingi milioni 5 pesa taslimu kila mmoja au bondi mbadala ya shilingi milioni 10
Maafisa wa Tume ya maadili na kupambana na ufisadi walimkamata Gikonyo siku ya jumatatu . EACC imekuwa ikimchunguza Gikonyo kwa mali ambayo hajaweza kueleza yenye thamani ya shilingi milioni 600 katika kipindi cha miaka mitano .
Afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak kupitia taarifa amesema maafisa wa tume hiyo wamekuwa wakimchunguza afisa huyo wa zamani wa KRA pamoja , mkewe wake Lucy Kangai na kampuni yao ya biashara kwa jina Giche Limited.