Maneno ya mwisho ya Bob Collymore kwa Patrick Quarcoo

Afisa mkuu mtendaji wa Radio Africa Patrick Quarcoo alikuwa mwandani wa marehemu Bob Collymore, ambaye kufikia kifo chake alikuwa afisa mkuu mtendaji wa Kampuni ya Safaricom.

Quarcoo alitoa hotuba iliyojaa hisia kali akieleza nyakati za mwisho akiwa na Collymore na mambo ambayo alimweleza kabla ya kuaga dunia. Ujumbe wake ulinata nyoyo za waliohudhuria hafla ya maombi ya kusherehekea maisha ya mwenda zake Collymore siku Alhamisi.

Quarcoo alikuwa miongoni mwa marafiki wa karibu sana na Collymore waliyoenda kumtembelea nyumbani kwake siku ya Jumapili saa chache tu kabla ya kifo chake kilichoacha wengi vinywa wazi.

Je, marehemu Collymore alimweleza nini quarcoo?

"Kusema kweli sifamahu sana mambo ya ahera na mbinguni, lakini ikiwa kuna mapepo kama wanavyosema nikifa nitarudi kucheza cheza na pazia za nyumba yangu," Quarcoo alimnukuu Collymore 

Aliendelea kusema

"na ikiwa kuna maisha baada ya kifo, basi katika hafla yoyote ya wanangu mkiasha misumaa nitakuja kuipuliza, mkiasha tena nitapuliza tena ishara kwamba bado nipo".

Katika ujumbe wake pia, Quarcoo alisema kwamba Bob aliwasihi sana kutomuacha mkewe Wambui na wanawe atakapokuwa ameaga dunia.

"Nitafurahi sana ikiwa nitapewa siku tatu zaidi za kuishi, lakini nawaomba msimame na Wambui."

Kifo cha Bob ni pigo kwa wengi wakiwemo watoto aliokuwa akifadhili masomo yao ambao kwao Bob alikuwa 'baba'.

TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO