Maombi na Limau yaponya Corona - Magufuli asema

Kwa mara nyingine tena rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuwa maombi na kunywa maji ya Limau ama Lemon yanaweza kuponya virusi vya corona.

Magufuli amesema kuwa maombi na maji hayo yamemfanya mwanawe kupona virusi hivyo baada ya kuambukizwa na kwa sasa anafanya mazoezi.

“Nina mtoto wangu alipata corona, mtoto wa kuzaa mimi, amejifungia kwenye chumba akaanza kujitibu, akanywa malimau na tangawizi, amepona yuko mzima sasa anapiga push up," alisema Magufuli.

Alisema haya alipokuwa anahudhuria misa ya kanisa katika kanisa la Lutherana Tanzania.

Jumamosi, rais Kenyatta alifunga mpaka wa Kenya na Tanzania kufuatia ongezeko la visa vingi vinavyoripotiwa katika mipaka hiyo.

Kama njia ya kujibu hatua hiyo, Tanzania iliamua mizigo yote inayotoka Kenya kuwekwa katika mipaka yake.

“I thank religious leaders who have been praying to God to lead me during this pandemic. So you can see the trend how Lord, our God, has responded to our prayers,”  Magufuli alisema.

Kwa sasa kiongozi huyo wa Tanzania anapania kutenga siku zingine tatu za maombi katika taifa hilo kama njia ya kumshukuru Mungu.

Amesema kuwa visa vyote vya maambukizi katika taifa hilo vinapungua katika hospitali zote.

Magufuli ameongeza kuwa hatafunga shughuli zote katika taifa kwani itachangaia pakubwa kuzorota kwa uchumi.

“Hatuwezi kubali corona itawale, Mungu wetu atatawala… tumekua na magonjwa kama ukimwi… (We can’t allow the virus to rule, our God will prevail ….we have had many diseases like HIV-Aids),"  alisema.