Nyota wa TV Lulu Hassan na mumewe Rashid Abdalla ni miongoni mwa wanandoa wanaopendwa sana nchini .
Wawili ha oleo wanaadhimisha miaka 11 ya ndoa na walifunga ndoa siku kama ya leo ,na ili kuadhimishasiku hii Lulu aliziweka picha zake na mumewe insta na kuandika ;
“It’s been a minute …Happy Anniversary to us Mwajita…and EID MUBARAK to all my muslim brothers and sisters”
https://www.instagram.com/p/CDSyVBxlhjW/
Kwa upande wake Rashid amesema uvumilivu na heshima ndio imekuwa nguzo ya ndoayao akisema ;
“#sisemikitu Mapenzi hayana sogora wala aliyebora cha msingi kuridhiana, kuvumiliana, kusitiriana, kuheshimiana na kuelewana. Asante Mungu kwa hapa tulipofika. Happy anniversary to us.”
Wawili hao wamejaaliwa watoto watatu – wavulana wawili na msichana mmoja .tazama picha zao