Mapenzi sumu: Mwanafunzi wa kidato cha 3 Ajiua baada ya mpenzi wake kumhadaa

Mwanafunzi katika shule ya mseto ya  Lumama huko Lugari amejiua  baada ya kugundua kwamba mpenziwe wa kike  ana mpenzi mwingine . Ripoti zaashiria kwamba mwanafuzi huyo wa kidato cha tatu alikunywa sumu  baada ya mpenzi wake aliye katika kidato cha pili  kugunduliwa kwamba ana mpenzi mwingine katika shule jirani .

Akithibitsha kisa hicho  chifu wa eneo la lugari Evans Adavachi  amesema mwanafuzi huyo aliamua kujiua baada ya kupata fununu kwamba msichana huyo alikuwa na  uhusiano mwingine wa kimapenzi na mvulana  wa shule jirani . Mvulana huyo aliaga dunia akipokea matibabu katika zahanati alikokimbizwa .