MAPICHA: Gidi amzawadi Ghost Mulee na jezi murwa kutoka Ufaransa

Mgeni njoo mwenyeji apone ni mojawapo ya misemo mingi ambayo inaashiria ukarimu, wema na upendo. Ijapokuwa yeye sio mgeni, mtangazaji Gidi alimnufaisha mwenzake, Ghost Mulee siku ya Jumatano baada ya kurejea nchini kutoka ziara yake ya bara uropa.

Gidi alirejea nchini mwishoni mwa juma lililopita baada ya ziara ya mwezi mzima ya bara Uropa, ambapo alibahatika kuzuru nchi kadhaa zikiwemo; Dubai, Ufaransa, uhispania na Italia kabla ya kurejelea majukumu yake ya utangazaji siku ya jumatatu.

Kando na ilivyokuwa uzoefu au mtindo ambapo Ghost Mulee ndiye aliyekuwa na juhudi za kumtunuku mwenzake Gidi kila alipotembelea nchi zingine, hatimaye Gidi alionesha ukarimu wake wakti alipomzawadi mwenzake na jezi murwa kutoka klabu ya kandanda ya Lyon, ya Ufaransa.

Mtangazaji huyo hakuwachia hapo kwani pia alimzawadi mzalishaji wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, bwana Justice Langat kofia maridadi kutoka Lyon pia.

Tazama picha hizi: