'Mara nyingi hatukuwa tunazungumza tukiigiza,' Wilbroda azungumzia uhusiano wake na Papa Shirandula

Awinjjja
Awinjjja
Charles Bukeko anayefahamika sana kama Papa Shirandula maeach urithi wake nyuma, aliaga dunia Mnomo JUlai 2020 kwa ajili ya virusi vya corona.

Wilbroda na Awinja waigizaji wenzake wakiwa kwenye mahojiano walizungumzia jinsi walivyokuwa wanajiandaa kwa uigizaji wao.

Akiwa kwenye mahojiano Wilbroda alisema,

"Kitambo sikuwa namfeel, katika siku zetu za kwanza katika set tulikuwa tunatofautiana sana wakati mwingine angesema ama kutenda vitu ambavyo sikukubaliana navyo

Wakati mwingi tukiwa tunaigiza hatukuwa tunaongea, hata salamu." Alisema Wilbroda.

Pia alifichua kuwa walipokuwa wanahitaji kuigiza wakipendana, hakuwa na la kufanya bali waliigiza na baada ya kuigiza wangerudi kuwa maadui.

"Lakini baada ya muda mnafahamiana vyema na bada ya muda kuyoyoma tulikuwa marafiki wa karibu kwa maana ni mtu ambaye nilikuwa na zungumza naye kila wakati

Nilihamia alipokuwa anaishi na urafiki wetu ukakua na tukakua marafiki wa kufahana."