Marcus Rashford kusalia Oldtrafford hadi 2023

Marcus Rashford
Marcus Rashford
Mshambulizi  wa Manchester United Marcus Rashford  amesaini mkataba wa malipo ya  £200,000 kwa wiki ili kusalia na kilabu hiyo hadi  Juni mwaka wa 2023 ,akiwa na chaguo la kuongeza muda huo kwa mwaka mmoja zaidi .

Nyota huyo wa England mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na  United  akiwa na umri wa miaka 7 na  kusonga katika vitengo vya Oldtrafford hadi mwaka wa 2016 alipoichezea timu kuu akiwa na umri wa miaka 18 . Amesema Manchester United  imemkuuza kama mchezaji na kama mtu huku akifurahia uamuzi wa kumpa  mkataba mpya wa kuichezea the Red Devils .

" Nitafanya kila niwezalo ili kuifanya kilabu hii kurejelea hadhi yake na kuipa mafanikio ambayo mashabiki wetu wanastahili’ amesema Rashford.Mzaliwa huyo wa Wythenshawe  Rashford  ameichezea   the Reds mechi 170  na kuiwakilisha England mara 32 .