Marianne Kitany afunguka A-Z jinsi simu ya Mithika Linturi ilisheheni picha za ngono

unnamed (2)
unnamed (2)
Mkewe seneta wa Meru Marianne Kitany amefunguka mwanzo mwisho kilichochochea kuvurugika kwa ndoa yake na mmewe Mithika Linturi katika kikao cha mahakama ya Milimani. Kitany anasema kuwa aligadhabishwa zaidi kipindi alipopata picha za uchi za mwanamke mwingine kwa simu ya mmewe. Hii iliashiria kuwa mmewe alikuwa na jicho la nje.

Soma mengine hapa:

Katika ushahidi wake mbele ya mahakama, Marianne ameeleza bayana kuwa aliichukua simu ya bwanake na kupekua mle ndani na kupata picha za uchi mwanamke mwingine aliyemtumia mmewe. Kitany alizidi kufunguka kuwa mmewe alikataa kufanya mapenzi naye kitu kilichopelekea yeye kuchukua hatua ya kutamatisha ndoa yao.

Aidha, Kitany aliwasilisha picha zinazoonyesha kuwa walifanya ndoa na sherehe ya kitamaduni . Alisimulia jinsi mmewe alimtishia na kuondoka wanapoishi huku juhudi za familia zikifanyika kuwaleta pamoja na kutafuta suluhu. Bwanake aliwahi kutuma wanapolisi kuja kumvurusha katika nyumba mtaa wa Runda.
Soma mengine hapa:

 Ndoa ya wawili hawa imekumbwa na kizungumkuti na balaa kubwa. Kitany alieleza mbele ya korti masaibu yote aliyofanyiwa na Mithika Linturi.