Martha Karua

‘Watu wako waliniibia kura,’ Martha Karua alimwambia Uhuru

Kinara wa Narc-Kenya Martha Karua, alifichua vile alimkabili kwa hasira rais Uhuru Kenyatta, baada ya rais Kenyatta kutaka kumteua katika baraza la mawaziri, pendekezo ambalo alikataa.

Karua alisema kwamba Uhuru alizungumza naye baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ugavana wa kirinyaga kwa gavana wa Anne Waiguru.

“Yalikuwa mazungumzo ya kibinafsi na rais alitaka kunipa wadhifa wa waziri na nikakataa. Nilimwambia kwamba sikuwa na hamu ya kuwa katika baraza lake la mawaziri kwa sababu watu wake waliniibia kura.

Mwenyekiti wa Jubilee tawi la Kirinyaga, Mureithi Kangara, alikuwa amemuomba rais Uhuru Kenyatta kumteua Karua katika baraza la mawaziri.

Karua kisha alikwenda mahakamani kutaka korti ibatilisihe uchuguzi wa Waiguru. Waiguru hata hivyo alishinda kesi zote kuanzia mahakama kuu hadi mahakama ya upeo..

Katika uamuzi wake jaji wa mahakama ya upeo Jaji Isaac Lenaola alisema kwamba Karua alishindwa kushawishi mahakama kwa kuthibitisha madai kwamba hongo ilitumiwa katika uchaguzi wa Kirinyaga wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017.

“Uamuzi wa mahakama ulikuwa wa mwisho, lakini nadhani haukuwa wa haki na hata wao wanajua hilo. Niliwasilisha ushahidi wangu kwa wakati ufaao, lakini kile mahakama ilisema ni kwamba niliwasilisha stabadhi kwa wakati unaofaa lakini walichelewa wenyewe kuushughulikia katika muda unaohitajika na kwamba hawawezi kunisaidia,” Karua alifoka.

Aliendelea kusema kwamba Waiguru hakustahili kuwa gavana wa Kirinyaga.

TAARIFA IMETFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO

Read here for more

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments