Mary Wambui Murder: Kucheleweshwa kwa dhamana ya washukiwa

Judy Wangui na Michael Githae
Judy Wangui na Michael Githae
Washukiwa wawili wakuu waliohusika na mauaji ya mwana biashara Mary Wambui Kamangara,wataweza kungoja tena kwa siku kumi na nne wakiwa rumande.

Hii ni baada ya mahakama kukataa waweze kuachiliwa kwa dhamana,watakaa kwa siku hizo ili mahakama iweze kubaini kama wataweza kuachiliwa kwa dhamana.

Judy Wangui mpenzi wa mume wake Mary Wambui, na dereva wa texi Michael Githae Jumatatu aliweza kukataa madai kuwa alimuuwa Kamangara na kuweza kutupa mwili wake maeneo ya Juja, kaunti ya Kiambu.

Kisa hicho kiliweza tokea Januari, na marehemu kuzikwa Jumamosi wiki iliyopita huku mazishi hayo yakiwa ya huzuni huku mume wake akiwa amemuandikia marehemu shairi ya kuhuzunisha.

Karatasi ya mashtaka ilisema kuwa usiku wa 26/27 Januari mwaka huu katika sehemu ya four ways barabara ya Kiambu - Nairobi wawili hao waliweza husika na mauaji hayo.

Waliweza kufika mbele ya mahakama kuhusu mauaji hayo na kisha mwili wa marehemu kupatikana ukiwa umetupwa eneo la Juja karibu na hoteli ya Courtesy Beach.

Bwana Githae ambaye ni mwenye Mipals Travels Adventures and Hire, aliweza kuwaambia wachunguzi wa kituo cha polisi cha Juja, ambao walikuwa wanachunguza mauaji hayo kuwa aliweza msaidia Wangui kuutorosha mwili wa marehemu Mary.

Lakini aliweza kukataa madai kuwa alihusika katika mauaji ya mwanabiashara huyo, wawili hao walikuwa wajibu mashtaka hayo Jumanne iliyopita lakini wakili wa mshukiwa Wangui Cliff Ombeta aliweza kuomba mahakama kesi hiyo iweze kucheleshwa kwa muda.

Wawili hao waliweza kupelekwa kizimbani baada ya dakika chache baada ya saa tano asubuhi kufika, kesi hiyo iliweza kumalizwa kwa dakika saba.

Mashtaka hayo yalikuwa yameongozwa na Christine Ndombi amabaye alikataa kuachiliwa kwa dhamana kwa washukiwa hao.

Na kumuuliza jaji Christine Meoli kupa mashtaka iweze kufaili jawabu kwanini washukiwa hao wazidi kukaa rumande na kueka kesi hiyo kando.

Bwana Sam Ogutu ambaye ana muakilisha Githae aliweza kuomba mahakama iweze kusikiza ombi hilo la kuachiliwa kwa dhamana lakini jaji Meoli aliweza kukataa na kusema kuwa mahakama imeshikana kwa sana.

Aliweza kuelekeza kuwa ombi hilo liweze kusikizwa machi 18 mbele ya mahakama, wachunguzi bado hawajabaini kama Kori ataweza kutoa kauli na ushahidi dhidi ya mpenzi wake Judy.

Readmore: