dj.evolve

Masaibu ya Babu Owino: Hali ya DJ Evolve, hahisi sehemu za mwili wake

Risasi ilikwaruza mfupa shingoni mwa DJ Evolve unaoungana na uti wa mgongo, habari kuhusu hali yake tangu alazwe baada ya kupigwa zimechipuka.

 

Babu Owino kusalia rumande hadi Jumatatu, akanusha mashtaka ya kujaribu kuua

DJ Evolve aliyedaiwa kupigwa risasi na mbunge wa Embakasi East Babu Owino atafanyiwa upasuaji kwa mara ya tatu. Kulingana na Mike, rafiki wa karibu wa DJ Evolve, uti wake wa mgongo ulikwaruzwa na kupelekea kupoteza uwezo wa kuhisi katika sehemu ya chini ya mwili wake na kufanya miguu yake kuwa dhaifu.
FELIX AMEKUWA AKIIMARIKA KUTOKANA NA MATIBABU NA HALI YAKE NI THABITI. KUFIKIA JANA ALIKUWA ANAUMWA SANA NA HANGEWEZA KUSONGESHA SEHEMU YA CHINI YA MWILI WAKE,LAKINI YEYE MWENYWE ALINIAMBIA KWAMBA ALIKUWA ANAHISI KWA MBALI BAADHI YA SEHEMU AMBAYO NI ISHARA NZURI YA KUREJESHA HISIA ZOTE ZA MWILI..

dj evolve
Mike alisema kwamba wageni wataruhusiwa kumwona kupitia kiyoo kuambatana na ushauri wa daktari.

DJ Evolve: usimamizi wa B Club wazungumzia madai ya kupigwa kwake risai na mbunge Babu Owino

KWA HIVYO ANATARAJIWA KUFANYIWA UPASUAJI WA TATU TUATUMAI NI WA MWISHO NA MTU YEYOTE ATAKAYETAKA KUMUONA ATAMUONEA KUPITIA KIOO KULINGANA NA USHAURI WA DAKTARI. HUKU TUKIPIGANIA HAKI, WACHA PIA TUMUOMBEE NA FAMILIA YAKE WAKATI HUU MGUMU. MUNGU AKUBARIKI!.

 

emabkasi east aspirant babu owino

Babu Owino atasalia korokoroni hadi Jumatatu wakati mahakama itapoamua kuhusu ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments