Masaibu ya kumwunga Ruto mkono: Mbunge Kimani Ngunjiri adai kuhangaishwa kwa sababu ya Ruto

KIMANI 2
KIMANI 2
Mbunge wa bahati Kimani Ngunjiri amesema kuondolewa kwa walinzi wake na kutakiwa kurejesha bunduki aliopewa na serikali ni hatua inayolenga kumnyamazisha yeye na wabunge wanaomwunga mkono naibu wa rais William Ruto .

Akizungumza katika afisi ya DCI ya Nakuru alipowasilisha bunduki yake na bastola  Mbunge huyo ameishtumu serikali kwa kuwahangaisha viongozi wote ambao wameonyesha nia ya kumsaidia Ruto kumrithi rais Uhuru Kenyatta baada ya mwaka wa 2022 .

.

" Wanaweza kuzichukua bunduki zao na walinzi wao, hatutatikishwa, tutasema ukweli  kuihusu nchi hii’ amesema mbunge huyo mzushi .

Amedai kwamba polisi walimsingizia kesi ya uchochezi  kwa lengo la kumpokonya bunduki zake . Ngunjiri amehoji kulengwa kwake na serikali kwa kile ambacho tayari kinajulikana baada ya kuwekwa katika vyombo vya habari .

Siku ya jumatatu mbunge huyo  aliagizwa na DCI kurekodi taarifa kuhusu matamshi yake  yanayohusiana na kufurushwa kwa nibu wa rais William Ruto kutoka afisi yake ya Mombasa.

Ngunjiri  ni miongoni mwa viongozi  waliotakiwa kuzisalimisha silaha zao kwa polisi kwa kujihusisha na uhalifu. Magavana na wabunge wanaokabiliwa na kesi kortini kuhusu visa vya ukiukaji wa sheria wametakiwa kuzisalimisha bunduki zao na pia kupokonywa walinzi kwa ajili ya agizo lililotolewa na Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai .

Hatua hiyo inamaanisha kwamba magavana, wabunge au maafisa wa serikali wanaokabiliwa na kesi mahakamani watalazimika kutafuta ulinzi  mbadala na kutojihami .