Masaibu ya Man United na Tottenham, shida ni kocha ama wachezaji?

Mashabiki wa klabu ya Manchester United na Tottenham Hotspurs ni wenye ghadhabu baada ya klabu hizo kuandikisha matokeo mabaya kwa majuma matatu sasa katika ligi ya Uingereza, ligi ya Europa, na ligi ya mabingwa ulaya.

Mkufunzi wa klabu ya Man United amejipata katika upande mbaya wa mashabiki baada ya kupoteza mechi dhidi ya Newcastle wikendi iliyopita, tukio ambalo limechangia wao kwa sasa kushikilia nafasi ya 12 katika ligi ya Uingereza wakiwa na pointi 9.

Solsjaer hakuweza kushinda mechi nyingine katika ligi ya Europa dhidi ya klabu ya AZ Alkmaar baada ya kutoka sare tasa.

Katika ligi ya Uingereza, Solsjaer bado alitoka sare ya bao moja na klabu ya Asenali.

 Mechi zingine ambazo Solsjaer hakuweza kuandikisha ushindi ni:

WestHam vs Man United (2-0)

Southampton vs Man United (1-1)

Man United vs Crystal (2-1)

Mauricio Pochettino vile vile amejipata pabaya baada ya klabu hiyo ya Spurs kuadhibiwa vikali mabao tatu kwa bila na Brighton wikendi iliyopita, hivi sasa wakishikilia nambari 9 na pointi 11

Pochettino alipokea kichapo tena katika ligi ya mabingwa Ulaya baada ya klabu inayocheza ligi ya Ujerumani Bayern Munich kuwanyuka mabao 7-2 nyumbani kwao White Hart Lane.

Baada ya matokeo hayo duni, wa kulaumiwa ni wakufunzi ama wachezaji?