Masaibu Ya Onyango: Akosa kazi kwa kuandika CV yake Carriculum vitamin

Kwa mda sasa, kitengo ukipendacho cha 'Masaibu ya Onyango' kimekuwa kikiletwa kwako na Gidi kila asubuhi.

Kitengo hiki ambacho huangazia jamaa kwa jina Onyango, hutumika kusimulia mambo yanayomkumba Onyango kwani kama muigizaji wa sinema za Mr. Bean, shida na masaibu tele ndio humfuata.

Soma usimulizi wake Gidi.

Unajua onyango anakuanga na mambo mengi sana. Onyango alikuwa London, alikuwa anasomea law na amaemaliza na amerejea nchini. Unajua hii nchi yetu kupata kazi baada ya kusoma ni shida. Onyango ametengeneza CV ametembelea different law firms.

Amefanya application na ameenda interview, unajua wakili anafaa kuwa mkakamavu, yuko very smart. Sasa Onyango ile kamati ya interview imeketi pale na CV yake iko mezani. Kitu ikatokea, wale jamaa hawajazungumza bado na Onyango kuchungulia ile CV akaona alifanya makosa. Badala ya kuandika curriculum vitae, alikuwa ameandika curriculum vitamin!

Hapo Onyango akashindwa wameona hayo makosa kweli? Na unajua hapendi aibu ndogo ndogo. Hapo akasema kuwa hawezi endelea na interview na akatoka na kwenda kufungua biashara yake kwa jina Onyango and sons advocates.

Isitoshe siku yake ya kwanza kazini, alipokea mteja na kwa sababu alitaka kujipendekeza, kabla yule mgeni wake azungumze, Onyango alichukua simu na kujifanya kuwa anazungumza na mteja. Hapo alianza kusema kuwa wateja wake walioko New York hawawezi kumlipa kwani yeye hulipisha zaidi ya milioni moja.

Isitoshe katika ile harakati, alisema kuwa korti ilikubali kuskiza kesi yake na kuwa ana uwezo wa kutetea hata watuhumiwa wa mauaji.

Hata hivyo licha ya hayo yote alipozungumza na yule mteja kilichompata hakuamini. Kumbe hakuwa mteja ila fundi wa simu kutoka Safaricom.

Pata uhondo kamili.