masaibu.ya.onyango

Masaibu ya Onyango: “Rudishia bibi yako poster yake!”

Kama kawaida wajua kuwa kila siku ya wiki kabla ya kitengo cha Patanisho na story za Ghost Mulee, kuna kitengo murwa cha ‘Masaibu ya Onyango”.

Kitengo hicho spesheli huwa kimeandaliwa na huletwa kwako na mtangazaji, Gidi Gidi. Kitengo hiki huwa kumhusu jamaa kwa jina Onyango ambaye hukumbwa na masaibu kila uchao.

Masaibu Ya Onyango: Akosa kazi kwa kuandika CV yake Carriculum vitamin

Mara hii, Onyango ni boss ama mdosi maeneo ya Industrial area na yeye ndiye anafaa kuhakikisha kuwa mambo yanafanywa ipasavyo.

Kulingana na bwana Gidi ilifika mahali wafanyikazi wa Onyango wakaanza kumkosea heshima na lazima angetafuta mbinu ili arudishe ile hadhi yake, na kurudisha heshima kutoka kwa wafanyikazi wake.

“Akaamua atengeneze poster imeandikwa, ‘I am the boss’. Akaandika vizuri na kubandika nje ya ofisi yake kwa mlango na wafanyikazi wakipita walikuwa wanaona kile kibango.” Gidi alisimulia.

Aliongeza,

“Wale wafanyikazi wake wakipita wanaangalia na kuenda kando kumcheka wakisema, ‘Angalia haka kamtu eti sasa kanataka tukaogope?’.

Sasa kuna huyu mfanyikazi bwana Wafula ambaye ni mcheshi sana. Sasa alingoja Onyago saa zile ameenda kando kidogo na kuchukua kalamu, na hapo mahali palikuwa pameandikwa ‘I am the boss’ Wafula akaandika, ‘rudishia bibi yako poster’.”

Wakenya wasimulia masaibu waliyopitia mikononi mwa wazazi wao (AUDIO)

Tazama kanda hii,

 

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments