Hili limeibuka katika mkutano uliofanyika jumatatu kati ya uongozi wa senate ,hazina ya kitaifa na wdau wa ugatuzi ili kuidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 187 kuzuia kullemazwa kwa oparesheni za serikali za kaunti baada ya utata kuzuka kuhusu fumo unaotumiwa kagawa pesa hizo .
Gazeti la The Star limegundua kwamba maseneta 25 ambao wiki jana waliongoza kuangushwa kwa mswada wa serikali kupuitisha mfumo huo pamoja na marekebisho yaliyopendekezwa wanapanga tena kuyakataa mapendekezo yaliyotolewa ili kumaliza utata huo .
Marekebisho hayo yametolewa na kiranja wa wengi katika senate aliyeungwa mkono na rais Kenyatta na Kiongozi wa ODM Raila Odinga .
Wakiwa ni maseneta 25 wanaopinga marekebisho hayo ,maseneta hao wamezidi idadi ya maseneta 24 waaohitajika kukataa mfumo huo ambao utazifanya kaunti 18 kupiteza jumla ya shilingi bilioni 17
Utata huo sasa umejaa sarakasi za kisiasa huku naibu wa rais William Ruto akiwashawishi wafuasi wake kuukata mfumo huo .
Siku ya jumapili Raila alikuatana na baadhi ya washirika wa Uhuru wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe nyumbani kwa katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli .
Katika mkutano huo Raila aliwahakikishia washirika hao wa rais kenyatta kwamba mrengo wake utaunga mkono mfumo huo .
Seneta wa Siaya James Orengo ambayeni kiongozi wa wachache katika senate alipewa jukumu la kuhakikisha kwamba kundi la Odinga linatekeleza matamnio yake kuhusu kura ya mfumo huo