Maseneta wakosa kukubaliana kuhusu ugavi wa pesa

uHURU RAILA
uHURU RAILA
Pendekezo la kutaka  mfumo wa tatu wa kugawa pesa kwa kaunti kuahirishwa  kwa miaka miwili limekataliwa na maseneta  katika kura iliyopigwa siku ya Jumanne .

Hatua hiyo imejiri huku seneta wa Siaya James Orengo akimshtumu rais kwa ‘kutoweza kufikiwa ‘ kwa urahisi ili kuweza kushughulikia utata huo ambao umezua mgawanyiko katika senate .

Ripoti hiyo ya kamati ya fedha na  bajeti  ilikuwa imeunga mkono mapendekezo ya tume ya ugavi wa mapato CRA   ambayo yangezifanya kaunti zeney idadi yajuu yaw tau kupata mgao mkubwa na zenye idadi ndogo ya watu kupata kiasi kidogo  yalitaka mfumo huo kuanza kutekelezwa katika mwaka wa kifedha wa 2021/2022.

Hata hivyo  mapendekezo hayo ya seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata yalikataliwa na maseneta wenzake waliopiga kura kupinga hatua hiyo .

Jaribio hilo la senate siku ya Jumanne lilikuwa la sita kwa masenate kujaribu kupitisha mfumo huo mpya kuhusu jinsi pesa za kaunti zitakavyogawanywa .

  Maseneta walionekana kuunda mirengo yao ndani ya unge ili kukaidi ushauri wa viongozi  wa vyama  vyaoa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga waliotaka mfumo huo kupitishwa .