Maseneta wapinga hatua ya kuweka kiwanda cha nyama (KMC) chini ya idara ya jeshi

Mseneta siku ya Almhisi alasiri walikosoa vikali hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuweka usimamizi wa kiwanda cha nyama cha KMC chni ya idara ya jeshi nchni (KDF).

Hoja ya kupinga mabadiliko hayo iliwasilishwa katika seneti na seneta wa Machakos Boniface Kabaka. Seneta maalum Abshiro Halake aliunga mkono hoja hiyo akisema kwamba ni mkondo hatari kuanza kuwaachia wanajeshi usimamizi wa mashirika ya serikali.

“Je jeshi letu sasa ni la kutengeza nyama, je Jeshi letu sasa ni shirika la kusaka masoko ya nyama?’’ Halake aliuliza.

Seneta wa Kilifi Stewert Madzao na mwenzake wa Mandera Mohamud Maalim, walisema kwamba KMC imekuwa ikidorora kutokana na changamoto za uhaba wa wateja na kwa hivyo kulikuwa na haja sana kuibinafsisha ili kuleta nguvu mpya na kubadili mwelekeo wa shirika hilo.

“KMC inafaa kubinafsishwa na kuiondoa kutoka minyororo ya usimamizi mbovu. Kwa miaka mingi sasa huu ndio umekuwa mjadala na ulikuwa katika mipango ya serikali wakati wa rais Mwai Kibaki," Maalim alisema.

Soma habari zaidi hapa: