Maseneta wapitisha mfumo wa ugavi wa mapato kwa kaunti

Maseneta 41 siku ya alhamisi wamepitisha  mfumo  utakaotumiwa kuzipa fedha kaunti baada ya meizi kadhaa ya utata .

Maseneta  hao walipitisha kwa kauli  moja  ripoti ya wenzao 12 waliokuwa wamepewa jukumu la kuafikia mfumo ambao utakubaliwa na kaunti zote .

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameahidi kuzipa kaunti shilingi bilioni 50 katika mwaka ujao wa kifedha na kurahisha kazi ya kupatikana kwa mwafaka wa kukubaliwa na wote .

Kakamati iliyosimamiwa kwa pamoja na maseneta Johnson Sakaja na Moses Wetangula ndio iliyoafikiwa mfumo huo .

Mfumo huo uliopendekezwa unatilia  mkazo vigezo  vinane  mgao wa mwanzo(asilimia 20) idadi ya watu(asilimia 18) afya (asilimia 17) kiwango cha umaskini(asilimia 14) kilimo(asilimia 10) barabara(asilimia 8,ardhi (asilimia nane) na miji(asilimia tano)

Katika mfumo mpya  Nairobi ndio itakayopewa mgao wa juu  wa shilingi bilioni 18 baada ya kupewa bilioni 3.3 za ziaa .kaunti nyingine zenye migao ya juu ni  Nakuru (Sh2.5 billion), Kiambu (Sh2.2 billion)  na Turkana (Sh2 billion).

Mgao wa Lamu umeongezeka hadi shilingi bilioni 3.1 ilhali  Tharaka Nithi imeongezwa shilingi milioni 289. Hakuna kaunti inayopoteza pesa katika mfumo huo mpya