Mashabiki wamwonya Chipukeezy kuhusu uhusiano wake na Kibanja

Ukimuuliza mchekeshaji Chipukeezy atasema kuwa lazima wakenya wazungumze. Jina lake kamili ni Vincent Muasya  Mutua.

Wakenya wengi wamekua wakimwonya chipukeezy kuhusu uhusiano wake na mpenziwe Kibanja  kwenye mitandao yake ya kijamii, Chipukeezy amekuwa akimweka mpenziwe kama status mara kwa mara huku akionesha jinsi penzi lake lilivyo noga na kipenda roho chake

Hata hivyo, wakenya wengine wakimwonya dhidi ya tabia za kumweka wazi mpenziwe kuwa huenda wakaachana hivi karibuni.

"Nakupenda pia mpenzi. "Kibanja  akijibu moja ya picha zake chipukeezy. Wakenya walichukua nafasi hio kumkumbusha mvunja mbavu Eric Omondi jinsi alivyoweka wazi uhusiano wake kabla haujaingia mchanga.

"Eric Omondi aliachwa sa wewe ni nani uturingie hapa kila siku."

"Kaka Mapenzi ya mitandaoni haidumu."