Mashabikia washabikia hatua ya Samidoh kushirikiana na Sauti Sol

Wiki moja tu baada ya wanamziki wa kikundi cha Sauti Sol cha humu nchini kuzindua albamu yao ya Midnight Train,sasa mmoja wa kikundi hicho Bien,amefichua kuwa watashirikiana  na mwanamziki wa humu nchini Samidoh kutoa nyimbo.

Wakenya baada ya kuona jumbe hizo wameshabikia hatua hiyo wengi wakihoji kuwa wanasubiri kuona namna ushirikiano huo utakavyofanya.

 

Miaka michache katika tasnia ya muziki nchini japo msanii Samidoh ambaye ni afisa wa polisi nchini ametega anga na kujipata akiwa na mashabiki wengi wanaoshabikia nyimbo zake.

Bien alikuwa wa kwanza kutuma ujumbe na kuandika ;Mtajificha wapi?

Wengine walikuwa na haya ya kusema

Kate actress : Tumalizeni uuuuui 👐 👐 👐

Cate kaddy : You want to kill us now, huh?

Myk mukka : Rhumba Mugithi tukisonga

Tracy Waithera : Tuuukunyweni kabisa

Jayc ; I’m not ready to die out of good music

Dj Shiti : wataficha vichwa wapiii!!

Samidoh muchoki : itakuwa moto kama pasi ya makaa nani 🔥 🔥

John articles : Ghafla bin vuu 🔥 🔥 🔥 😂 😂

The Sarah Mwangi : Wowowowo hapa ndio mugithi na rhumba meet time make our lives happy