Gavana wa Kitui Charity Ngilu amepata pigo baada ya mahakama kukataa kuzuia kuwasilishwa kwa hoja ya kumuondoa afisini.
Ngilu alikuwa amewasilisha kesi kortini Juni tarehe 24 akitaka kupata maagizo ya kuwazuia wawakilishi wa kaunti dhidi ya kuuwasilisha bungeni mswada wa kumuondoa mamlakani.
Jaji Welson Korir siku ya Alhamisi amesema ombi la Ngilu halikuwa na msingi wa kutosha wa kushurutisha kutolewa kwa maagizo aliotaka
Korir pia amesema ombi hilo liliwasilishwa Nairobi na sio katika kaunti ya Kitui.
Jaji ameongeza kwamba ni muhimu kwa wakaazi wa kaunti iliyoathiriwa waweze kufika mahakamani kufuatilia kikao kinachoendelea kuhusu uongozi wa kaunti yao.