Mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini, Nigeria yachukuwa hatua

Serikali ya Nigeria imemuita balozi wa Afrika Kusini nchini humo kuhusu mashambulizi na wizi unaolenga raia wa kigeni mjini Johannesburg.

Nigeria inadai kwamba biashara zinazomilikiwa na raia wake zinalengwa katika mashambulizi hayo na kusema kupitia twitter kwamba “enough is enough”.

Nchi zingine za Afrika tayari zimewatahadharisha raia wao kuhusiana na hali tete nchini Afrika kusini.

Maafisa wa serikali nchini Afrika Kusini wameshtumu hali nchini humo kwa makundi ya kihalifu na sio ubaguzi dhidi ya raia wa kigeni.

Wabunge watatu watiwa mbaroni wakizuru msitu wa Mau

Siku ya Jumatatu, watu kadhaa walikamatwa mjini Johannesburg baada ya kuzuka kwa ghasia huku maduka yakivunjwa na bidhaa kuibwa huku majumba na magari yakiteketezwa. Polisi walilazimika kutumia gesi za kutoa machozi, risasi za mipira na silaha zingine nyepesi kutuliza hali.

Katika taarifa balozi wa Nigeria nchini AfrikaKusini alitaja hali hiyo kama “utovu kabisa wa sheria” na kutoa wito kwa raia wa Ngeria nchini Afrika Kusini kupiga ripoti kuhusu matukio wanayokumbana nayo.

Ubalozi wa Ethiopia umeshauri raia wake kufunga biashara zao wakati huu wa taharuki.