Masharti ambayo Jowie anapaswa kufuata baada ya kuachiliwa

Leo ikiwa siku ya alhamisi, bwana Joseph Irungu almaarufu Jowie ameachiliwa huru kwa dhamana ya kitita cha shilingi milioni 2 katika kesi ya mauji ya mwanabiashara Monicah Kimani.

Jowie aliachiliwa huru na mahakama ya Milimani.

Jowie aliachiliwa huru baada ya Jaji James Wakiaga kusema hakuna sababu ya kumnyima mshtakiwa dhamana akiongeza kuwa tayari hali zimebadilika.

Mashahidi ambao walikuwa chini ya ulinzi tayari wametoa ushahidi wao.

Hata hivyo Jowie alipewa vikwazo kadhaa kufuatia kuachiliwa kwake;
1. Amezuiwa kuzungumza ama kutoa maoni kuhusu kesi hiyo katika mtandao wa kijamii au mahala popote.
2. Anapaswa kuripoti kwa chifu kila mwisho wa mwezi.
Jowie alikamatwa Septemba 25 mwaka uliopita ambapo alikuwa rumande wakti wa sherehe za krismasi mwaka wa 2019.
Juni mwaka uliopita, mahakam ilikataa kumpa dhamana kwa mara ya pili.