Mashemeji Derby: Gor na AFC Leopards kufufua uhasimu wao wikendi hii

Gor Mahia na AFC Leopards watafufua uhasimu wao wikendi hii watakapochuana kwa mara ya kwanza msimu huu katika ligi ya KPL. Msimu uliopita mabingwa hao wa KPL waliwafunga Ingwe mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya msimu kabla ya kuwanyuka 3-1 na kutwaa taji hilo kwa mara ya 18.

Mashemeji Derby imekua karamu kwa Gor katika siku za hivi majuzi ikizingatiwa kua Leopards hawajawahi kuwafunga mahasimu hao tangu mwaka wa 2016.

Na tukitua ulaya, Real Madrid wanajitayarisha kuwasilisha ofa kwa Manchester City kumnunua Raheem Sterling na ofa ya pauni milioni 70 na kubadilishana na Gareth Bale.

Wawakilishi kutoka Real watasafiri kuangalia mchezo wa Sterling Uingereza mwezi ujao, akiwa nyumbani Montenegro na ugenini akiwa Kosovo, kabla ya kuamua ofa yao kwa City.

Wawakilishi wa Sterling walikutana na mkurugenzi mkuu wa Real Jose Angel Sanchez msimu wa joto katika jitihada zilizotibuka, za kumtaka kiungo huyo wa City kuhamia Bernabeu.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amemshtumu meneja wa Manchester City Pep Guardiola baada ya kumlaumu Sadio Mane kwa kucheza vibaya.

Mane, kiungo wa Liverpool na Senegal, alipewa onyo jumamosi wakiwa Aston Villa kwa kucheza visivyo, kabla ya kufunga bao la kichwa na kuwahakikishia the Reds ushindi wa 2-1.

Guardiola alinukuliwa akisema kua mara nyingine Mane hucheza vibaya na mara nyingine ana talanta ya kufunga mabao dakika za mwisho matamshi ambayo yalimchukiza Klopp.

Jitihada za Chelsea katika ligi ya mabingwa zimepigwa jeki na ripoti kuwa N'Golo Kante yuko tayari kuregea katika kikosi kitakachopambana na Ajax leo usiku.

Mfaransa huyo hajakua tangu walipowanyuka Southampton 4-1 katika ligi ya Primia kutokana na jeraha la mguu lakini kocha Frank Lampard amefichua kuwa sasa yuko tayari kucheza. Kante alifanya mazoezi na kikosi hicho jana, wanapomalizia matayarisho kabla ya mechi hiyo.

Tottenham wamepinga kadi nyekundu aliyopewa Son Heung-min kwa kumgonga Andre Gomes, na kumpelekea kupata jeraha baya la mguu.

Gomes alifanyiwa upasuaji jana na Son alitokwa na machozi siku ya jumapili alipoona jeraha hilo ugani Goodison Park. Awali refa alikua amempa Son kadi ya njano kabla ya kuibadilisha na kumpa nyekundu. Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kiungo huyo hakukusudia kumjeruhi Gomes na anaamini VAR ingefaa kutumika.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester United Bastian Schweinsteiger amependekeza kua Jose Mourinho anataka kuchukua nafasi ya meneja wa  iliyo wazi. Miamba hao wa Ujerumani walimwachisha kazi meneja Niko Kovac juzi baada ya kufungwa mabao 5-1 na Eintracht Frankfurt.

Schweinsteiger, anasema Mourinho amekua akimuuliza maswali mara kwa mara kuhusu Bayern na hata amekua akijifunza kijerumani.