Akizungumza na n waandishi wa habari siku ya alhamisi katika makao makuu ya KICD Magoha amesema kundi la maafisa kutoka mashirika mbali mbali ya serikali litaunda mwongozo na mikakati ya kuwawezesha walimu kutoa mafunzo ya kijamii kwa wanafunzi .
" walimu watawapa wanafunzo masomo kuhusu uadilifu chini ya muundo wa nyumba kumi . TSC iatoa mpango huo ambao hautawagharimu wazazi chochote’ amesema Magoha
Katika elimu ya msingi , wadau katika sektaya elimu wamesema licha ya mafunzo kutolewa kwa njia ya redio ,runinga na kupitia mtandao ,kuna wanafunzi wengi ambao hawawezi kuyapat mafunzo hayo .
Wizara ya elimu na TSC zikitumia kundi la pamoja na idara mbali mbali za serikali pamoja na machifu sasa litatumia mpango wa Nyumba kumi ili kufanikisja masomo hayo ya ‘kijamii’
mpango wa Nyumba Kumi ulianzishwa kupitia agizo la rais na kuwekwa katika gazeti rasmi la serikali kama njia moja ya kukabiliana na ukosefu wa usalama wakati visa vya ugaidi na uhalifu vilipoongezeka mwaka wa 2013.
Magoha ameongeza kwamba vyuo vingi vikuu na vya mafuzoya elimu ya juu haviko tayari kufunguliwa na vitaslaia kufungwa hadi januari mwaka wa 2021 . Ameongeza kwamba serikali imetenga fedha za kuwalipa walimu walioajiriwa na bodi za shule ,maafuisa wa ulinzi na kulipa gharama kama vile maji na umeme katika shule za umma