Mass testing kuanza rasmi wikendi hii-Rais Kenyatta asema

NA NICKSON TOSI

Akizungumza kwa mahojiano na stesheni za redio za kiswahili humu nchini, Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa kupimwa kwa umma kuanza rasmi wikendi hii katika maeneo ambayo yameathirika kwa wingi.

Amesema  kuwa maeneo ambayo yataangaziwa zaidi ni kama halmashauri ya bandari nchini KPA, na maafisa wa afya ambao wamekuwa kwenye mstari wa mbele kupigania uhai wa wale walioathirika.

Mass Testing yaanza rasmi Mombasa -Maafisa wa afya wasema

Wakati uo huo, rais Kenyatta aliwataka wakenya kuzingatia sheria ambazo serikali imeweka ili kukabiliana na janga la Corona.

Huku hayo yakijiri  hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret imeanza kufanyia watu vipimo vya sampuli kuhusiana na virusi hivyo.

Mass testing Kuanza! Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema

Hospitali hiyo ilipokea vifaa vya kufanikisha mchakato huo kutoka taasisi ya KMTC na itakuwa na uwezo wa kufanya vipimo vya watu takriban 96 baada ya saa 8.

Kufikia sasa serikali imewafanyia vipimo watu zaidi ya 14000.