Mass Testing yaanza rasmi Mombasa -Maafisa wa afya wasema

NA NICKSON TOSI

Kutokana na idadi ya kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona kuripotiwa katika kaunti ya Mombasa, maafisa wa afya hii leo wameanza rasmi kuwafanyia vipimo wakaazi wa kaunti hiyo ili kubaini idadi ya watu walioathirika.

Zoezi hilo linaazimia kupima zaidi ya watu 5000, wakianza na wafanyakazi wa halmashauri ya bandari nchini KPA baada ya wafanyakazi wa halmashauri hiyo kufariki kutokana na virusi hivyo.

Wasimamizi wa KPA wamesema zoezi hilo linatarajia kuwapima aghalabu watu 1,000 ambao wanafanya kazi ndani ya halmashauri hiyo.

Meneja mkuu wa KPA Rashid Sallim amesema wafanyakazi 157 wanaofanya katika sekta ya afya wamefanyiwa vipimo na matokea yao yatatolewa Jumanne.

Mass testing Kuanza! Waziri wa afya Mutahi Kagwe asema

Wiki KPA ilithibitisha kuwa maafisa wake 7 walikuwa wamepatikana na virusi hivyo.

Kufikia sasa taifa la Kenya limesaji visa 270 vya maambukizi huku watu 67 wakiwa wamepona na 14 wakiwa wameaga dunia .