Massawe Japanni anusurika baada ya kuhusika katika ajali mbaya (PICHA)

Mtangazaji Massawe Japanni, yuko salama salmini baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika eneo la uwanja wa kitaifa wa Nyayo, Nairobi.

Gari la massawe aina la Nissan X-trail, liligongwa vibaya baada ya gari la abiria la Orokise sacco (Ongata-Rongai- Kiserian) kumgonga kutoka nyuma.

Dirisha la nyuma ya gari lake lilivunjwa lote huku taa la nyuma la upande wa kushoto kubondwa vibaya.

Tulipozungumza na mtangazaji huyo wa Bustani la Massawe, alituhakikishia kuwa yupo salama ilhali bado ajali hiyo imemuacha na mshtuko mkuu.

"Niko salama lakini bado nimeshtuka." Alisema Massawe.

Sasa hivi, mama huyo wa wasichana watatu yuko katika kituo cha polisi cha eneo la viwanda (Industrial area) ambapo ameenda kupiga ripoti.

Tunatuma pole zetu kwa Massawe Japanni na tunamtakia kila la heri, na pia tunamshukuru mola kwa kumlinda na pia kulinda abiria ambao pia walihusika kwa ajali hiyo.

Kwa wapendwa wa Bustani la Massawe twaomba mtuwie radhi huku tukimuombea dada yetu.