Mastaa waliovunja uhusiano wao na klabu zao kimabavu

Payet
Payet
Dirisha la usajili linaelekea kukamilika na hivyo basi kunao mastaa wanatazamiwa kuvigura vilabu vyao wakati huu kwa ajili ya kujiingizia pesa ndefu ama kwa ajili ya kujitakia sifa.

Neymar alilazimisha uhamisho wake kutoka klabu ya Barcelona na kujiunga na miamba wa Ufaransa PSG ila kwa sasa kitubua kimeingia mchanga.

Barani Ulaya tumeshuhudia mastaa wakilazimisha uhamisho kutoka klabu moja hadi nyingine ila baada ya uhamisho wakabaki kuwa makopo tu.

Thibaut Courtois

Mlindalango huyu anayekipigia Real Madrid kwa sasa alikuwa ngome muhimu ugani stamford Bridge baada ya kukamilisha mkopo wake na klabu ya Atletico Madrid. Hata hivyo, mwaka 2017, Courtois aligoma kupiga mazoezi na timu ya kwanza ya Chelsea ili aruhusiwe ajiunge na klabu ya Real Madrid. Msimu wa kwanza ugani Santiago Bernabue Courtois alijipata matatani baada ya kutoa mpira wavuni mwake kwa zaidi ya mara 34 ambayo ni mengi zaidi ya nusu aliyokuwa amefungwa msimu wa 2016/2017.

Dimitri Payet

Baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya Mersaille ya Ufaransa, Payet alijitabulisha kuwa kipenzi cha wengi ugani London Stadium huku akiwachangamsha mashabiki wa klabu ya Westham na kuwapa hamu ya  ushindi kwa mara nyingine. Januari mwaka 2016, Payet na mkufunzi wa Westham, Slaven Bilic walikosana jambo lilopelekea Payet kuandika barua akitaka kuigura klabu hio. Kama ilivyo kwa Courtois, Payet aligoma wiki mbili jambo lilopelekea WestHam United kumuza tena klabuni Mersaille.

Phillipe Coutinho

Kiungo huyu mshambulizi wa Barcelona alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Kandanda ugani Anfield jambo lilopelekea mkufunzi wa Liverpool, Jurgen Klopp kumfanya naibu naohadha wake. Hata hivyo, mabwenyenye wa Barcelona walikuja na pesa ndefu jambo lilomfanya Coutinho kuchanganyikiwa. Baadaye, Coutinho aliandika barua akitaka kukubaliwa ajiunge na Barcelona licha kwamba klabu yake haikuwa tayari kumuachilia. Kwa sasa hatma yake Coutinho imo mashakani ugani camp nou na huenda akalazimika kutafta malisho kwingineko.

Diego Costa

Diego Costa anatabulikana kwa kupenda vurugu uwanjani licha ya kuwa yeye ni chui mbele ya lango. Baada ya kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza, aliyekuwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte alimwambia Fiego hamuhitaji jambo lilopeleka Costa kugoma kurejea Uingereza akidai auzwe au sivyo hatocheza tena. Baada ya vuta nikuvute nyingi, Costa aliishia kujiunga na Atletico Madrid na msimu uliopita alicheka na wavu mara tatu pekee.

Laurent Koscienly

Koscienly ameigura klabu ya Arsenal baada ya miaka tisda ugani Emirates. Mlinzi huyu mwenye umri wa miaka 33 alikuwa beki tegemezi kwa zaidi ya miaka minane hadi akawa nahodha wa kikosi hicho. Hata hivyo, mwezi juni mwaka huu, Koscienly aligoma kusafiri na Arsenal na kulazimisha uhamisho kwenda klabu ya Bordeaux ya Ufaransa. Kilichotia chumvi zaidi ni jinsi alivyojiwasilisha klabuni hapo baada ya kuvalia jezi ya Arsenal na kisha kuivua na kubaki na jezi yake mpya.