‘Mat of death’:DCI  Yawanasa wahudumu wa matatu waliomwua abiria kwa kumsukuma .

Idara ya DCI imewakamata  wahudumu wawili wa matatu  waliomsukuma abiria kutoka gari lililokuwa mbioni na kumwua . Polisi wamesema gari hilo nambari ya usajili  KCC 021A limenaswa  kufuatia kifo cha  Gerald Kimondo. Wawili hao   Naphtali Fondo mwenye umri wa miaka  33 na Alex Gikonyo mwenye umri wa miaka 20  walimsukuma  mwendazake kutoka gari  hilo lililokuwa mbioni na kusababisha kifo chake .

Kisa hicho kiliripotiwa kutokea  agosti tarehe mbili mwaka huu  katika barabara kuu ya Thika karibu na Roysambu baada ya abiria huyo kutofautiana na washukiwa hao wawili . Kimondo aliaga dunia papo hapo baada ya kusukumwa .  kondakta wa basi hilo alitorka  baada ya tukio hilo lakini  basi lenyewe likanaswa na dereva kukamatwa .Baadaye dereva aliachiliwa huru  baada ya siku mbili katika hali ya kutatanisha . Ilidaiwa aliachiliwa huru kwa bondi ya polisi yenye thamani ya  shilingi elfu 60  pamoja na basi hilo kwa jina zam zam .

OCPD  wa Kasarani Peter Kimani  alipoulizwa kuhusu  kuachiliwa kwa dereva huyo na basi ,alisema  liliondolewa hatia . “ Utaratibu wa trfaiki ni kuwa gari linaposababisha ajali ,ukaguzi unafanywa na kisha linaachiliwa .lakini kesi hiyo inaendelea’ amenukuliwa akisema OCPD huyo .