Wakati Moi alipokuwa mamlakani uongozi wake ulikuwa wa kupigiwa mfano, kwa sababu hangewacha mwenye makosa akae na makosa hayo bali alikuwa anawahadhibu ipasavyo.
Baadhi ya watu waliotiwa kizuizini wakati wa uongozi wa hayati Moi ni hawa hapa;
Wakili John Khaminwa
John ni wakili katika mji wa Nairobi, aliponea chupuchupu baada ya kuandamwa hadi kwa boma lake na helkopta ya wanajeshi mnamo juni 4/1982 na kufikishwa katika afisi kuu za CID na kuachiliwa mnamo oktoba 12/1983.
Raila Amolo Odinga
Mwaka wa ,1983 aprili,14 Raila alitiwa kizuizini na watu wengine na kunakili yote yaliyopitiwa wakiwa ndani.
Maina wa Kinyatti
Juni,7,1982, mhadhiri wa chuo kikuu alikamatwa kwa uchapishaji taarifa za uchochezi. alifungwa kwa miaka sita kwa kosa hilo.
Kamoji Kang’aru Wachira na Edward Akong’o Oyugi
Mwaka wa 1982,Julai,24 wahadhiri hao wawili walitiwa kizuizini, walikuwa wahadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi
Wachira alifunza jiografia naye Edward alifunza somo la saikologia katika chuo hicho.
Koigi wa Wamwere
Alikuwa mbunge wa Nakuru alipotiwa mbaroni agosti,12,1982 kwa kuwa katika kikundi ambacho kilifahamika kama 'Six Bearded Sisters'
Kenneth Matiba
Ni mwanasiasa ambaye alipatwa na ugonjwa wa papasa baada ya kufungwa gerezani wakati wa uongozi wa Moi kutokana na msimamo wake wa kukashifu uongozi uliokuwepo wakati huo uongozi uliotajwa kama wa kikoloni.
Alikuwa gerezani 1990 Julai.
Kwa hakika Moi alifanya kazi yake kwa ustaarabu wake na mwelekeo mwema.