Vikwazo vya usafiri huenda vikaondolewa na serikali baada ya uzinduzi wa mwongozo wa taratibu za utalii ,afya na usalama .
Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i amesema taifa sasa lipo salama kwa usafiri . Matiang’I amesema serikali itazidi kuimarisha usalama na kusimamia shughuli zote za uangalizi ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona .
Amesema hali ilivyo sasa itawalazimu wakenya kujifunza kuishi na virusi vya corona huku juhudi za ulimwengu mzima kutafuta tiba zikiendelea .
Kauli yake hiyo imekaririwa pia na waziri wa Afya Mutahi Kagwe.serikali ilisitisha usafiri wa aina yoyote wa kimataifa mwezi aprili ili kuthibiti maambukizi ya covid 19 .