Matiang’i amelalama kuhusu idadi ya juu ya watu wa makosa madogo katika seli akisema hatua hyo sasa inaigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kuwashughulikia . Aliyasema hayo Jumanne wakati wa uzinduzi wa mwongozo kuhusu mashtaka katika taasisi ya mafunzo ya mashtaka ,Loresho .
Amesema jela na rumande zina watu wengi ambao kesi zao zinaweza kusuluhishwa kwa haraka kupitia njia mbadala za kusuluhisha mizozo .
“ iwapo mwongozo huu utafatwa ,idadi ya watu wa maosa madogo katika jela na rumande itapunguzwa’ amesema
Kwa mfano mtu anayekiuka sheria za trafiki hulipa faini ya shilingi 600 ilhali kumweka rumande kutagharimu zaidi ya shilingi 30,000 .
Matiang’i alisifu sana mwongozo huo akisema utazuia kuwekwa seli kwa watu ambao kesi zao zinaweza kushghulikiwa nje ya mahakama haraka na kuokoa pesa za serikali kwalengo la kuhakikisha kwamba ni kesi zenye ushahidi na za kutafuta haki kwa walalamishi zinazopewa uzingativu .
Mwongozo huo unamhitaji mwendesha mashtaka kutathmini ubora wa usahhidi wake kabla ya kuamua kuendelea na kesi mahakamani .