Matokeo ya upasuaji, Msimbojeni wa vidole na kucha watoa dalili za kunasa wauaji

unnamed
unnamed
Hasimu wa Tob Cohen walivunja fuvu lake la kichwa, mguu wa kushoto na baadaye wakavunja mifupa ya mikono yote miwili.

Katika muda huu wote Tob alikuwa anang'ang'ana kujinusuru kutoka kwa maadui hawa.

Upasuaji unaonyesha kwamba Cohen alipitia kifo cha uchungu sana.

Soma hadithi nyingine;

Chembechembe za msimbojeni uliofanyiwa vidole na kucha zake unaonyesha njia iliyo na mwangaza kuwapata wauaji hawa.

Mwili wa Cohen ulipatikana umetupwa katika tanki wiki iliyopita ijumaa.

Hii ni baada ya wiki 8 tangu apotee ghafla.

Tanki hii ilikuwa imevukiwa kwa ardhi nje ya jumba lake katika mtaa wa Kitisuru.

Mwili wake ulikuwa umefunikwa kwa sandarusi nyeusi.

Soma hadithi nyingine;

Cohen aliripotiwa kupotea kutoka nyumba yake iliyopo Lower Kabete kati ya Julai 9 na Julai 20.

"Mabaki ya mwili wake yanaonyesha dalili za kusukumiwa mateso." Walisema polisi.

"Mikono,miguu na shingo zilikuwa zimefungwa kabla kuuawa. Wauaji hawakuwa na haraka katika tukio hili." Alisema George Kinoti wiki iliyopita ijumaa.

Upasuaji huu ulisubiriwa sana na ukaweza kufanyika jana katika hifadhi ya wafu ya Chiromo.

Mjane Sarah Wairimu ambaye anakisiwa kuwa alihusika katika mauaji ya mmewe alikuwepo.

Soma hadithi nyingine;

Waliokuwepo wengine ni dadake Tob,Gabrielle Cohen, maafisa wanaopeleleza kisa hiki na jamaa wa familia.

Sarah alikuwa chini ya ulinzi mkali kipindi hiki chote cha upasuaji.