Video ya dakika 47 iliyorekodiwa ya Peter Ngugi aliyekuwa akiwapasha polisi habari akikiri kuhusika na mauaji ya wakili Willie Kimani haitachezwa kortini .jaji amesema afisa aliyerekodi video hiyo hakufutwa kanuni zifaazo wakati wa kuichukua video hiyo iliyofaa kutumiwa kama ushahidi .
Miili ya wakenya walioaga dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Ethiopia airlines imewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA ili kuchukuliwa na jamaa zao .miili 28 kati ya 32 ya wakenya hao walioafriki katika mkasa huo imewasili mapema leo katika uwanja huo .watu 157 waliangamia katika ajali hiyo mwezi machi .
Uhaba wa walimu huko taita taveta unachangia kudorora kwa ubora wa elimu .mbunge wa mwatate Andrew Mwadime aniataka tume ya kuwajiri walimu TSC kuwaajiri walimu zaidi katika eneo hilo kwani kuna vijana wengi waliohitimu kuwa walimu lakini hawana kazi .
Mbunge wa kitui mashariki Nimrod Mbai anataka kamishna wa kaunti ya Kitui John Ondego ahamishwe kwa madai ya kukosa kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo linaloshambuliwa mara kwa mara na wafugaji wa ngamia . Mbai amesema wenyeji sasa wamelazimika kuishi katika kambi za muda ilhali serikali haijachukua hatua zozote madhubuti za kuwalinda .Odengo hata hivyo amekana kuwyatelekeza maslahi ya wakaazi hao.
Chama cha ODM kimetakiwa kuwahakikishia wakenya kwamba kitadumisha amani wakati wa uchaguzi mdogo wa kibra .mbunge wa kiharu Ndindi Nyoro amesema kisa kama kilichotokea mwishoni mwa wiki ambapo msafara wa mgombeaji wa Jubilee Mcdonald mariga ulishambuliwa kwa mawe sio jambo linalofaa kukubaliwa .
Serikali itazidisha mara dufu jitihada za kukabiliana na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mwaka huu .afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la mihani Mercy Karogo amewashauri maafisa wakuu wa elimu katika kaunti ndogo kuhakikisha kwamba wanafuatilia kikamilifu usimamizi wa zoezi la mtihani katika maeneo yao .
Wakaazi wa Mombasa wanaitaka serikali kuboresha usalama katika feri ili kuzuia maafa siku za usoni . wamesema baadhi ya sehemu za feri zinafaa kuboreshwa na pia kuweka vifaa vya kuwawezesha watu kujiokoa wakati panapotokea dharura .