Eliud and Kipchoge-compressed

Matukio ya Spoti Wikendi: Tazama jinsi Kenya ilivyotamba ulimwenguni

Imekuwa wikendi ya kufana sana katika ulingo wa spoti baada ya Wakenya kuonyesha ubora wao ulimwenguni  mzima na  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionyesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Haya ni baadhi ya matukio muhimu yaliyosababisha bendera ya Kenya kupeperushwa ughaibuni:

 

Eliud Kipchoge – Ineos 1:59 Challenge

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Ulimwengu ulishuhudia mkenya Eliud Kipchoge kuwa binadamu wa kwanza duniani kukimbia mbio za kilomita 42 chini ya masaa mawawili.

Kipchoge ambaye alikata utepe baada ya saa 1.59.40 aliweka historia katika ulingo wa riadha kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza riadha hiyo katika kuda huo.

 

Timu ya raga ya 7s kwa kina dada yafuzu kwenye Olimpiki 2020

Aidha, wachezaji wa raga 7s kina dada waliwapiga wenyeji Tunisia katika nusu fainali na kufuzu katika michuano ya Olimpiki ya Tokyo Japan manmo 2020.

Timu ya  raga ya 7s ya kina dada imejipatia tiketi ya kushiriki katika Olimpiki ya Tokyo Japan 2020, baada ya kufuzu katika  fainali ya mashindano hayo nchini  Tunisia Jumapili.

Kenya ambao  ni mabingwa watetezi waliwapiga  wenyeji Tunisia 19-0 kwenye  michuano ya nusu finali  na  kujikatia tikiti  ya moja kwa moja kwenda Japan

Timu hiyo ya Kenya, maarufu kama Lionesses   ilikuwa timu ya nane kufuzu kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020.

 

Lawrence Cherono Ashinda Debele

Lawrence Cherono aliibuka mshindi katika mbio za marathon chicago kwa muda wa saa 2:05:45. Alikata utepe   kwa sekunde moja kutoka mbele ya  Debela amabye aliibuka wa pili.

Mengstu alikuwa wa tatu karibu kwa muda wa 2:05:48. Kinyume na ilivyokuwa na mbio za wanawake,  ushindano baina ya wanaume ilikuwa pambano la karibu zaidi.

Mo Farah na Karoki waliondoka nje ya mashindano  hayo kabla kabla ya raundi ya mwisho, wakiwaacha Cherono, Debela na Mengstu waking’ang’ania  ushindi wakiwa mstari wa kumalizia.

 

Rekodi ya 2003 yavunjwa na Brigid Kosgei

Brigid Kosgei  ndiye bingwa wa dunia katika marathon ya kina dada  baada ya kumaliza katika muda wa 2:14:04, zaidi ya dakika sita mbele ya Ababel Yeshaneh, ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 51, na Gelete Burka ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 55 wakati Ethiopia ilimaliza la pili na la tatu.

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments