Kabwe amesema wananchi wanafaa kuambiwa ukweli kuhusu taswira hasili ya jinsi mambo yalivyo. Taifa hilo lilisajili visa 30 zaidi siku ya Jumatano na kufikisha jumla ya visa 284 vya watu walio na coronavirus
Waziri mkuu wan chi hiyo Kassim Makaliwa Jumatano aliwarai wananchi kuiamini serikali na wataalam wake wa afya katika vita dhidi ya ugonjwa huo. Majaliwa alisema serikali mwanzo itatathmini hatua zifaazo kabla ya kuamua kutangaza mikakati kabambe ya kuweza kuzuia usambaaji wa virusi hivyo. Mikutano na misongamano ya watu katika hafla za kidini bado imeruhusiwa na rais Magufuli amenukuliwa akisema kwamba virusi vya Corona haviwezi kufaulu katika mwili wa kristu na kuwahimiza watu kufanya sala na maombi
Rais Magufuli amefutilia mbali uwezakano wa kutoa tangazo la kutotoka nje katika mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam ambako visa vingi vya ugonjwa huo vimeripotiwa.
Amesema tangazo kama hilo litavuruga kabisa uchumi katika jiji hilo la bandari linalotegemewa kwa kiasi kikubwa cha pato la nchi