Matumizi ya pesa zenyewe ndio hatufahamu! Kenya yapokea bilioni 78 kutoka IMF

usd-2874026__340
usd-2874026__340
NA NICKSON TOSI

Shirika la Kimataifa la Kutathmini matumizi ya pesa International Monetary Fund IMF limethibitisha mgao wa fedha kwa taifa la Kenya wa bilioni 78 kutumika katika vita dhidi ya coronavirus .

Zikiwa zimetumwa kwa wizara ya afya, bilioni izo za pesa zinatarajiwa kusaidia serikali kulipa baadhi ya madeni ya wizara hiyo na kusaidia kununua vifaa muhimu vya kutumiwa na wahudumu wa afya.

Kando na ufadhili huo pia Kenya inatarajia kupokea kitita kingine cha pesa takriban  bilioni 106 kutoka kwa benki kuu ya dunia ili kutumiwa katika mchakato wa kupigana na virusi vya Corona.

Bilioni hizo sasa kutoka IMF zitakuwa nguzo muhimu japo serikali imetuhumiwa vikali na wananchi kutokana na ubadhirifu wa mikopo hiyo inayotoka katika mashirika ya kimataifa.

Siku za hivi karibuni, waziri wa afya Mutahi Kagwe alilazimika kuelezea kamati ya bunge ya afya kuhusiana na matumizi ya pesa hizo.